Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Thursday, July 28, 2016


Mwanamuziki wa Nigeria anayeunda kundi la Psquare Peter Okoye ameomba msamaha kwa washabiki kufuatia ugomvi na kaka yake.
Kupitia video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii amesema timu nzima ya Psquare kwa sasa imerudi tena pamoja.
Akiwa amevalia kofia ndani ya gari, video hiyo inamuonesha Okoye ni mwenye kujuta, akisema kuwa anabeba jukumu kwa yote yaliyotokea.
Peter alikuwa na uhasama na pacha wake Paul, ambaye ndiye amekuwa akiimba naye kwa zaidi ya muongo mmoja, hali iliyofanya kugawa kundi hilo.
Kulikuwa na dalili kwamba utengano wao huo unahatarisha mafanikio ya mapacha hao.
Peter na Paul ambao wanapiga muziki wa hiphop wametoa nyimbo nyingi zilizovuma ndani ya Nigeria na nchi nyingine za Afrika.source BBC

0 comments:

Post a Comment