Lauryn Hill si mfungwa tena,mwanachama huyo wa zamani kundi la Fugees ameachiwa kutoka gerezani baada ya kutumikia kifungo cha miezi mitatu kwa makosa ya ukwepaji kulipa kodi.
Chanzo kimoja kimesema Lauryn Hill aliachiwa kutoka gerezani mapema siku ya ijumaa.Tunataarifiwa kwamba Lauryn Hill ameachiwa siku chache kabla ya kumaliza kifungo kwa sababu alikuwa mtii.
Lauryn Hill alianza kutumikia kifungo tangu July 8 baada ya kukutwa na makosa ya kukwepa kulipa kodi inayokadiliwa kuwa kiasi cha dolla millioni 1.8 ya mapatoa kwa miaka ya 2005 na 2007.
Sunday, October 6, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment