WIki iliyopita Kanye West alilalamikia Nike kutompatia heshima anayostahili kama balozi wao kupitia Air Yeez,mahusiano kati ya Kanye na Nike yalionekana kufikia mwisho pale Kanye alipowachana jukwaani katika moja ya matamasha yake ya hivi karibuni kwa kusema,mkurugenzi wa Nike bwana Mark Parker anamfanya mtoto.
Knye West aliongelea mahusiano yake na Nike na katika kituo cha Hot 97 na mtangazaji Angie Martinez,na kusema,katika kipindi cha miaka 5 nimedizaini aina 2 za sneaker za Air Yeez,tatizo kubwa ni malipo,hawanilipi kama wanavyowalipa donge nono wanamichezo wengine wanaowatangazia NIke.Ningeendelea kuvaa na kutiangaza Nike ila kwakuwa sasa nna binti na nna familia,wacha niangalie maslahi.
Kanye West amesema nageukia kufanya kazi na Adidas,bado haijawa rasmi ila ndiyo mpango uliopo na wote mnajionea jinsi ntavyoongeza mauzo ya Adidas kama,ntakuwaTupac wa Adidas na ntakuwa Hip Hop designer wa kwanza nifikie levo za mkwanja za akina“Jay Z na Diddy l.”
Tuesday, November 26, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment