Rapa toka Atlanta Jeezy anauanza mwaka 2014 vibaya,ripoti zinadai rappa huyo amekamatwa na polisi kwa makosa mbalimbali ya ukatili.
Ripoti zaidi zinadai tukio lililotokea huko Atlanta linamuhusu Jeezy na mwanaye mpaka kufikia polisi kuhusishwa.Rapper Young Jeezy yupo mikononi mwa polisi huko Atlanta kwa makosa ya ukatili dhidi ya mtoto wake wa kiume,mtandao wa TMZ unasema kutokana na documentsza mashitaka zinaonyesha,Jeezy alimpiga mtoto wake kuanzia bafuni ambako inasemekana alimgongesha katika vioo vya mlango,kisha akamrusha nje na kama haitoshi akaendelea kumrushia makonde usoni kisha akamrusha kitandani na kuziba pumzi kwa mto huku akimwambia ntakuua,ntapasua kicha chako kwa bastola.Inasemekana mtoto allifanikiwa kumponyoka baba yake na kukimbia lakini bodyguard wa rappa huyo walimblock.Baada ya Jeezy kushikiliwa kwa muda mfupi,alijidhamini mwenyewe kwa kutoa dolla 45,000.
Tukio la kukamatwa rappa Jeezy limetokea Tuesday (January 7) baada ya kujipeleka mwenyewe,tunataarfiwa tukio lilitokea mwaka 2012. Loya wa Jeezy amesema watakaa kifamilia kumaliza tatizo na kisheria.
Wednesday, January 8, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment