Sean "Diddy" Combs ametangaza kubadili jina na kulirudia jina lake la zamani,jina ambalo alilitumia kwa miaka mingi kiwa katika muziki,Puff Daddy,Diddy ametangaza uamuzi wa kulirudia jina lake la zamani wakati anatangaza mpango wa kuachia solo album yake ya MMM. Hivi karibuni Puff Daddy ameachia kipande cha upcoming music video ya "Big Homie," track ambayo iitaachiwa hivi karibuni.
Puff Daddy kama mwanamuziki ameshafanya kazi nyingi zilizopfanya vizuri zikiwemo album yake ya kwanza ya mwaka 1997,No Way Out. mwaka 1999 Forever,mwaka 2001 The Saga Continues..., 2002 We Invented The Remix,2006 Press Play na 2010 Last Train To Paris,ambayo aliachia akiwa na Dirty Money (Dawn Richard na Kalenna Harper).
0 comments:
Post a Comment