Mtandao wa TMZ umeandika,mwanamuziki wa rnb Chris Brown ataendelea kusota jela mpaka mwezi June.Brown ambaye alijukuta akiingia jela mwezi uliopita baada ya vitendo vya viovu katika kituo cha rehab na ataendelea kuwepo jela akisubiria kesi ya tukio la DC la yeye na mlinzi wake kumshambulia mtu.
Taarifa zaidi zianasema kesi ilikuwa isomwe leo lakini imeahitrishwa mpaka mwezi June.
Brown alijaribu kumuomba aachiwe huru kwa dhamana hakimu anayeendesha kesi ya kumpiga Rihanna lakini maombi yake yaligonga mwamba,hivyo hivi karibuni Brown atapelekwa huko L.A.ambako atakuwa jela mpaka mwezi June ambapo ataletwa tena
D.C. akiwa ndani ya dege la Con air ambapo tunataarifiwa ina mazingira ya ovyo kuliko economy.
Kama Brown atakutwa na makosa katika kesi ya kumjeruhi mtu huyo huko D.C,hakimu anayeendesha kesi dhidi ya Rihanna anaweza kumhukumu Brown miaka 4 gerezani.
0 comments:
Post a Comment