Jarida la People huchapishwa kila wiki nchini Marekani na kusomwa na watu wanaokaribia milioni 40
Jarida hilo limemtaja Mkenya Lupita Nyong’o kama mwanamuke mrembo zaidi duniani mwaka 2014.
Lupita ambaye alishinda tuzo ya Oscar kwa
uigizaji wake katika filamu '12 years a slave,' yuko kwenye ukurasa wa
juu zaidi wa makala ya wiki hii ya jarida hilo.
Katika orodha yake ya wanawake 50
warembo duniani,Lupita amewapiku waigizaji maarufu akiwemo Kerry
Washington, ambaye pia alishiriki katika filamu hiyo na mwanamuziki Pink
ambao walikuwa katika nafasi ya 10 na 5 mtawalia.Stacy Kiebler ambaye alisifika sana kwa kuwa na
uhusiano wa kimapenzi na muigizaji nyota George Clooney, alishikilia
nafasi ya nane.
Tuzo hii ya kivyake kwa muigizaji huyo imegonga vichwa vya habari nchini Marekani tangu kushinda
Mtandao wa People.com, unasema kuwa muigizaji
huyo alifurahia sana kutajwa na jarida hilo kama mwanamke mrembo hasa
kwa sababu wasichana kama yeye watapata kuwa na matumaini ya kufanikiwa
maishani kama yeye.
"Nimefurahi sana na hii ni fursa kuwafanya wasichana wengine wajihisi kuwa wana uwezo wa kufikia chochote maishani mwao.
0 comments:
Post a Comment