Rais Uhuru Kenyatta ametia saini sheria hio licha ya malalamiko kutoka kwa vikundi vya wanawake nchini humo.Taarifa kutoka katika ofisi ya Rais
ilisema kuwa mswada huo ambao unaojumuisha vipengee kadhaa kuhusu ndoa ,
imekuwa sheria sasa.
Mswada huo ulioleta mageuzi katika sheria ya
sasa , ilipitishwa na bunge mwezi jana kuidhinisha rasmi utamaduni wa
ndoa ya zaidi ya mwanamke mmoja.
Wakati mswada huo ulipopitishwa mwezi jana , wabunge wanawake waliondoka bungeni kwa Hasira baada ya mjadala mkali.
Viongozi wa baadhi ya makanisa pia wamepinga vikali mswada huo.
Shirikisho la kitaifa la mawakili wanawake pia limesema kuwa litapinga sheria hiyo mahakamani.
Katika sehemu nyingi barani Afrika, kuoa zaidi
ya mwanamke mmoja ni jambo la kawaida katika tamaduni nyingi sawa na
hali ilivyo nchini Kenya
Wednesday, April 30, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment