Ikulu ya ya Marekani imeijia juu kampuni ya simu ya Samsung kwa kutumia picha ya Rais Barack Obama aliyojipiga na mchezaji maarufu wa American professional baseball,David Américo Ortiz Arias, aka "Big Papi",anayechezea timu ya Boston Red Sox ya nchini Marekani kama tangazo la kibiashara.
Taarifa zaidi zinadai Samsung iliisambaza katika mtandao wa kijami wa Twitter kwa wateja wake na watu milioni 5.2 wanaoifuata kwa Twitter.Picha hiyo ilipigwa na Ortiz mwenyewe akiwa na Rais Obama akitumia simu yake ya Samsung mapema wiki hii.Msemaji wa Ikulu ya White House, Jay Carney, alisema kuwa picha ya Rais haipaswi kwa njia yoyote kutumiwa kwa sababu za kujinufaisha kibiashara.
0 comments:
Post a Comment