The Coachella ni tamasha la sanaa na Music linalofanyika kila mwaka siku 3 za mwisho wa wiki kwa wiki 2 mfurulizo na hufanyika huko California,Colorado Desert.Tamasha hili huanza mida ya saa 3 asubuhi na kumalizika saa 12 jioni.
Na haya ndiyo matukio yakukumbukwa katika tamasha la Coachella 2014
Mc toka pande za Chicago,Chance the rapper kumleta jukwaani pop star Justin Bieber na kuimbia naye collabo yao ya track "Confident" .
Tukio la Solange kumleta jukwaani Byeonce kwa kushtukiza alipokukuwa akitumbuiza wimbo wake wa "Losing You."
Pharrell pia alitumbuiza na hits zake alizotengeza kuanzia "Get Lucky" ,"Blurred Lines" hadi ngoma yake gumzo ya "Happy,"Na baadaye aliwashusha mastaa kibao akiwamo Gwen Stefani akaimba "Hollaback Girl" na Snoop Dogg aliyechengua na "Drop It Like It's Hot".Pharrell pia aliwadondosha mastaa kama Nelly, Busta Rhymes, Tyler the Creator ambao wote amefanya nao kazi.
Nas liyekuwa akisherekea miaka 20 ya albamu yake Illmatic aliwaacha hoi mashabiki waliohudhuria tamasha hilo kwa kumdondosha jukwaani mtu ambaye alishakuwa hasimu wake mkubwa miaka ya 2005,Jay Z.
OutKast hii ilikuwa mara yao ya kwanza baada ya miaka 7 kuimba pamoja ikawa kama ni tukio la kihistoria na kama haitoshi wakawaleta jukwaani wanamuziki wenzao tokea Atlanta,Janelle Monae rappa Future .
0 comments:
Post a Comment