Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Friday, July 11, 2014


Mnamo mwaka 1995,Jabbar Collins aliiona dunia chungu na mbaya baada kutajwa kuwa ni muuaji wa mtu aliyetambulika kwa jina la Rabbi Abraham Pollack na kuhukumiwa kifungo cha maisha.
Collins akiwa gerezani chini ya uangalizi mkali kwa takribani miaka 17 alijitahidi kuhangaikia rufaa na ndipo ilipokuja kujulikana ukweli baada ya ushahidi kukamilika na kuonekana bwana Collins hakuhusika na mauaji na hana makosa baada ya rufaa yake kutajwa jana na jaji Faviola Soto katika mahakama ya jiji la New York.
Akiwa nje ya mahakama Collins aliongea na waandihi na kuwaambia hukumu na kifungo ilikuwa chungu na sasa kama ni tamu.Chungu kwasababu nilifungwa bila kosa na wakati nikitukia kifungo nilifiwa na mama yangu,tamu kwasababu sasa nipo huru na nimepewa fidia kubwa ya dolla za kimarekani millioni 2 sawa na shilingi millioni 495,000,000 za kitanzania.

0 comments:

Post a Comment