Rappa wa MMG amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu mpaka sita kwa ufunjifu wa sheria akiwa chini ya uangalizi.
Mtandao wa TMZ,
umeandika,rappa MeekMill,27 alikuwa mahakamani huko Philadelphia siku ya ijumaa mchana kusikiliza kesi yake iliyotokana na tukio lake la mwaka 2009 kukamatwa na madawa ya kulevya na silaha.
Hakimu amesema Meek aliandaa matamasha mara kwa mara bila kutoa taarifa kama alivyotakiwa na akabadilisha namba ya simu bila kuitaarifu mahakama na kama haitoshi rappa Meek Mill alimtolea kauli chafu mkuu wa wilaya kupitia Twitter.
Meek akijitetea na kumtaka hakimu asimfunge aliiambia mahakama kwamba anategema kipaji chake kuisaidia familia yake inayomtegemea na September 9 anampango wa kutoa albamu Dreams Worth More Than Money.
Saturday, July 12, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment