Lil Eazy-E amesema anachokiona ni kwamba Ice Cube ana m bania na kuzizima ndoto zake za kuigiza filamu ya N.W.A. ukizingatia yeye ni damu ya aliyekuwa mwanachama wa kundi hilo,Eazy-E .
Lil Eazy ameuambia mtandao wa TMZ kwamba angekuwapo baba yake (Eazy-E ) lazima angempatia nafasi hiyo kwasababu anafanan naye na hata sauti na uongeaji wanafanana.
Chakushangaza Ice Cube amemchezesha mwanaye wa kiume,O'Shea Jackson Jr. kuigiza kama Ice Cube kitu ambacho angeweza kufanya hata kwa Lil Eazy.Lil Eazy ameongeza kusema pia anashangazwa kuona hata mtoto wa Dr. Dre hajashirikishwa.
Rappa Eazy-E alifariki mwaka 1995 baada ya kuugua ugonjwa wa AIDS.
Lil E ameongeza kusema hali hiyo haijamfurahia ila atasaidia kuitangaza kazi hiyo.i
Wednesday, July 2, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment