Neymar alirejea Brazil's training center wanapojifua wenzake wakisubiri kushindania nafasi ya tatu zidi ya Netherlands baada ya kuwa nyumbani kwa siku kadhaa akiugulia baada ya kuumia katika mechi dhidi ya Colombia , akiwa amevalia jezi ya Brazil,Neymar aliongea na waandishi wa habari na kuwaambia kwamba hii ilikuwa wiki mbaya zaidi kwake katika maisha yake.
Neymar pia alizungumzia kuumizwa na mchezaji wa Colombia,Carlos Zuniga,amesema baada ya tukio hilo Zuniga alimpigia simu na kumuomba msamaha,amemsamehe kwani anaamini ilikuwa ni katika ushindani wa kawaida kuwania mpira.
Neynar pia amesema alikuwa akiangalia mechi ya nusu fainali Brazil zidi ya Germany katika televisheni akiwa nyumbani lakini ilipofika dakika ya 79 ilimladhimu azime Tv baada ya timu yake kutandikwa bao la 7 - 1.
Neymar amesema Germany inakutana katika fainali na mahasimu wakubwa wa Brazil,Argentina, yeye atakuwa upande wa Barcelona mwenzake,Lionel Messi na Javier Mascherano .Sitoshabikia Argentina, nitashabikiwa wachezaji wenzangu wa Barcelona.
Argentina na Ujerumani sambamba na zawadi ya kombe la dunia,zitagombania dola milioni 35 kwenye mechi ya fainali mjini Rio De Janeiro.
0 comments:
Post a Comment