Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Saturday, July 5, 2014

Brazil star ruled out of World Cup (AP)

Mtandao wa BBC umeandika,nyota wa timu ya soka ya Brazil Neymar hatoshiriki tena katika michuano ya kombe la dunia baada kupata jeraha.
Mfupa wake unaoshikana na uti wa mgongo ilivunjika katika mechi ya ushindi wa mabao mawili dhidi ya Colombia.
Alibebwa na kutolewa nje akiwa katika machela lakini ametolewa hospitalini baada ya kufanyiwa matibabu.Neymar aligongwa upande wake wa nyuma dakika tano tu kabla ya mchuano huo wa robo fainali kukamilika.
Brazil pia itaendelea kushiriki katika mashindano hayo bila nahodha wake Thiago Silva katika mchuano wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani baada ya mchezaji huyo kupewa kadi ya pili ya Njano.
Kabla ya habari hizo za Neymar kutolewa raia wa Brazil walifurika katika barabara za taifa hilo kusherehekea ushindi wa timu yao.
Katika robo fainali ya kwanza Ujerumani iliishinda ufaransa kwa bao moja kwa bila .

0 comments:

Post a Comment