Gzaeti la Los Angeles Times limeandika,Usher atasherekea miaka 20 tangu kuachia albamu yake ya kwanza iliyobeba jina lake,Usher kwa kufungua sherehe za tuzo za MTV Video Music mwezi ujao.
Usher atafungua sherehe za tuzo za MTV Video Music za 31 mwezi August tarehe 24 huko Inglewood, Calif.
Usher alitumbuiza katika tuzohizo za VMA mwaka 2010 wakati huo akitamba na ngoma zake kali kama “DJ Got Us Fallin’ in Love” na “OMG.”
Mwezi uliopita alitumbuiza ngoma yake mpya ya “Good Kisser” katika tuzo za BET.
Sambamba na Usher muimbaji Ariana Grande atashambulia jukwaa kwa kutumbuiza ngoma yake iliyotengenezwa na producer Zedd “Break Free” .
Usher yupo katika maandalizi ya kuachia albamu yake mpya na ya 8 na mapema wiki hii ameachia ngoma nyingine toka katika albau hiyo aliyomshirikisha Nicki Minaj “She Came to Give It to You”.Usher ni jina la albamu ya kwanza ya mwimbaji wa R&B-pop wa Kimarekani - Usher. Albamu ilitolewa mnamo tar. 30 Agosti 1994 na studio ya LaFace Records na Arista Records.
Albamu ilipata kushika nafasi ya kwanza kwenye cha za Billboard 200 Bora. Usher pia ameshiriki kuandika mimbo minne ya albamu hii. Licha ya kupata mafanikio makubwa ya single zake, ni moja kati ya albamu zake zilizouza nakala ndogo iliyochini ya 50,000 kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment