Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Wednesday, July 9, 2014

 
Ujeruma imekuwa timu ya kwanza kufuzu kwenda Fainali ya kombe la dunia Brazil 2014 baada ya kuwaangushia kichapo wenyeji Brazil cha mabao 7-1 katika uwanja wa Estadio Mineirao ulioko Belo Horizonte.
Vijana wa kocha Joachim Low wameiadhibu Brazil na kuwa timu ya kwanza kuwahi kushindwa kwa mabao mengi zaidi katika hatua hiyo ya nusu fainali ya kombe la dunia.
Mbinu za makocha wawili wajerumani kuwashirikisha washambulizi Miroslav Klose,Thomas Muller na Mesut Ozil huku Schweinsteiger akiwaongoza Toni Krooos Khedira na Lahm katika kiungo cha Kati ndizo zilizoidhoofisha Brazil.Mechi Iliwachukuwa Wajerumani takriban dakika kumi tu za kwanza kupenya safu ya ulinzi ya Brazi.
Thomas Muller alifungua kalamu ya mabao kabla ya Klose kuidhibitishia Ujerumani fainali yao kombe la dunia kwa mkwaju uliomwacha kipa wa Brazil Julio Cesar asijue la Kufanya.
Klose kwa ushirikiano na Toni Kroos walifunga bao la tatu na la nne katika kipindi cha dakika moja.
Sami Kheidira alifunga la tano kunako dakika ya 29 kabla ya mchezaji wa akiba Andre Schurrle kufunga mabao ya 6 na ya 7 .
Bao la kufutia machozi la Brazil lilifungwa na Oscar kunako dakika ya mwisho ya mechi hiyo.
00:90 Oscar anaiifungia Brazil bao la kufutia machozi katika dakika ya mwisho ya mechi hii ya kihistoria .
Kufuatia kichapo hicho cha 7 - 1  nahodha wa Brazil David Luiz amewaomba radhi mashabiki wao.

 

0 comments:

Post a Comment