“Happy New Year,” ni filamu aliyoshirikishwa kutengeneza na kuigiza kinara starring Bollywood superstar Shah Rukh Khan, imevunja record ya mauzo ya nakala kwa siku ya kwanza nchini India record iliyowekwa na iliyokuwa inashikiliwa na filamu ya “Dhoom 3” iliyotoka mwaka 2013.
Filamu ya“Happy New Year” imetoka siku ya sikukuu ya mwaka mpya wa wahindi,(Diwali) na kuingiza kiasi cha dola za kimarekani 7.3 huko India siku ya ijumaa.
“Dhoom 3” iliingiza kiasi cha dola millioni 5.9 siku ilipotolewa na ilikuwa ni wakati wa sikukuu ya Christmas mwaka 2013.
filamu hiyo imeongozwa na Director Farah Khan ambaye pia aliongoza filamu ya Main hoon naa” na “Om Shanti Om,” ambazo zote aliigiza kinara Khan,katika filamu ya “Happy New Year” pia yupo kinara wa Bollywood heroine Deepika Padukone,Abhishek Bachchan na Boman Irani. Filamu hiyo imefanyika katika mazingira ya India na
Dubai.
Gharama za utengeneza wa filamu ya“Happy New Year” zinakadiliwa kufikia dola millioni 24 .
“Dhoom 3,” iligharimu dola millioni 20.
0 comments:
Post a Comment