Mkali wa mtindo wa rap Tanzania anayesifika kwa kuongea vitu kwa uwazi ama bingwa wa kuwachana,Ney wa Mitego amesema mwaka huu ataukamilisha kwa ngoma mbili.Aakiongea na mwandishi wa blogu hii Ney amesema,anataraji kuachia wimbo mwingine mwishoni mwa mwezi October chini ya studio yake mpya inayofahamika kwa jina la Free Nation chini ya producer mkali Mr T Touch ambaye amejipatia umaarufu mkubwa kutokana na kazi zake nyingi kufanya vizuri katika anga la muzii wa kizazi kipya.Ney ameongeza kusema mwaka huu inamladhimu atone nyimbo kwani mpaka sasa ameachia wimbo mmoja tu,Mr Ney na tayari ameshaufanyia video na sasa muda umefika wa kupakua kibao kingine.
Akiongelea studio za Free Nation,Ney amesema studio ndiyo kwanza mpya na atazindua kwa kuachia single yake na pia milango ipo wazi kwa wasanii wenzake kutumia studio hizo na producer Mr T Touch.
Pichani chini Mr T Touch,Ney wamitego na producer Shedy Clever:
Thursday, October 16, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment