Tamasha la Serengei fiesta Dar es salaam lililofanyika siku ya jumamosi tarehe 18/10 katika viwanja vya Leaders lilikuwa na mvuto na mashamsham ya aina yake.
Tamasha hilo lilipambwa na burudani toka kwa wasanii wa ndani ya nchi,nchi jirani kama Kenya,Nigeria na hata America.
Mashabiki wa muziki waliohudhuria tamasha hilo hawakuwa na ubaguzi katika kuwasapoti wasanii wote waliotumbuiza hasa wa nyumbani.
Kikubwa nilichokiona ni tofauti ya utumbuizaji ambacho wasanii wa Tanzania wanatakiwa kujifunza na kukitilia maanani ni,maandaliziutumbuizaji,namna ya kulitawala jukwaa na hata kuongea na mashabikina kuwasoma wanahitaji nini kwa muda huo,team work ya msanii kuanzia dj,dancers mpaka waimbaji wasaidizi.
Nikiangalia sioni tofauti kubwa sana kwa jinsi alivyotumbuiza rappa T,I toka marekani na Mwana Fa wa Tanzania,kikubwa ni rappa T,I alikuwa na timu inayojua nini cha kufanya,kuanzia dj wake na hata waimbaji wasaidizi tofauti na Mwana Fa ambaye alipanda yeye kama yeye bila ya kuwa na waimbaji wasaidizi wala dj wake.
Ukiachilia mbali burudani toka kwa wasanii wa nje na wa nchini kivutio kingine kikubwa kilikuwa na mandhari ya eneo la tukio,jukwa zurilililopambwa na taa za kutosha,Sund nzuri,mandhari ya backstage,mpangilio wa ratiba,kazi nzuri ya waendesha shughuli jukwaani,Mc B12 na ma dj wote akiwamo dj Zero.
Mwisho ningependa kuipongeza timu nzima ya waandaaji wa Serengeti Fiesta kuanzia Radio Clouds ,Primetime Promotion mkurugenzi wao bwana Joseph Kusaga,mkurugenzi wa ubunifu na uzalishaji bwana Ruge Mutahaba,na timu nzima iliyoshiriki katika maandalizi bila kuwasahau wadhamini Serengeti.
0 comments:
Post a Comment