Star wa miondoko ya pop na R&b Chriss Brown anatakiwa arudi kuendelea na mafunzo katika darasa la kujifunza kuzikabili hasira zake.
Chris Brown amewatolea maneno mbofumbofu watangazaji maarrufu wa kipindi cha Televisheni cha The Real, Tamar Braxton na Adrienne Bailon baadaya ya kumuongelea wakiwa katka kipindi.
Watangazaji hao jana jumatatu walikuwa wakijadili mambo ya udanganyifu katika mahusiano nandipo walipogusia kuzungumzia mahusiano ya Chris na mpezni wake wa sasa Karrueche,ambapo Tamar alisema mtu kama Chris hatakiwi kuwa mdanganyifu katika mahusiano sababu ni mtu maarufu na ni kioo cha jamii na kuongeza kusema:“I don’t think he’s a bad guy, I just think he’s young,”.
Adrienne pia aliongeza kusema kwa kupeleka lawama kwa Karrueche kwa kusema rafiki zake nao wanataka kutumia nafasi hiyo ya kumsogelea na hata kutembea na Chris Brown kwani nao wanautaka umaarufu na hata kuwa karibu kimapenzi na mtu maarufu”.
Baada ya kipindi hicho kurushwa , Chris aliingia katika akaunti yake ya Instagram na kuposti picha ya mtangazaji Adrienne na kuweka vipande vya video na ujumbe mrefu wa kuwakashifu na kuwachana.
Tuesday, November 4, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment