Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Wednesday, November 5, 2014

 
Katika hali ambayo tunaweza kusema siyo ya kawaida,mastaa Beyonce na mumewe,Jay-Z,Kanye West na wamefunguliwa mashataka dhidi ya wizi wa nyimbo.
Beyonce ambaye ni mke wa rappa Jay-Z amefunguliwa mashataka na  muimbaji msaidizi wake Ahmad Javon Lane ambaye anadai aliandika wimbo na kuupa jina "XOXO" na alimshirikisha muimbaji msaidizi mwenzake ambaye anafanya naye kazi kwa Beyonce.  
Katika maelezo yake katika mashataka amedai Beyonce ameuiba wimbo huo na kuuimba na kuubadilisha jina na kuuita "XO."
Muimbaji huyomsaidizi Ahmad Javon Lane ametaka mahaka imsaidie alipwe fidia ya kuibiwa wimbo wake ya dolla millioni3.
Tukiachana na Beyonce,mumewe Jay Z, Kanye West na Frank Ocean na wamefunguliwa mashtaka ya wizi wa wimbo na mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Joel Mac ambaye ameadai alikuwa akiuza cd zake nje ya hoteli waliyokuwa wakiishi mastaa hao miaka kadhaa iliyopita.
Joel Mac amesema alikuwa akiuza cd hizo nje ya hoteli ya Mercer Hotel kipindi ambacho mastaa hao walikuwa wakitengeneza albamu ya Jay Z' "Watch the Throne".
Katika mashataka aliyofungua Mac amesema kuna watu toka kwa hoteli hiyo akiwamo preoducer wa Jay-Z Mike Dean walinunua cd hiyo ambayo ilikuwa na wimbo aliouita Made in America ambao pia alisha ngaa kuuona katika albamu ya Jay Z siku chache baadaye na ilikuwa inafanan na ya kwake kuanzia beat hadi mistari.
Mac amitaka mahakama iwaamuru Jay, Kanye na Frank wamlipe sehemu ya faida ya mauzo ya albamu hiyo.

0 comments:

Post a Comment