Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Monday, November 3, 2014


Weusi ni kundi la muziki wa kizazi kipya wa hip hop/rap ambalo maskani yake ni Arusha na Dar es salaam japo linaundwa na wanachama wote wanaotokea mkoa wa Arusha.
Kundi la Weusi linaundwa na wasanii 5 toka makundi mawili,River camp na Nako II Nako Soldiers ambao ni Lord Eazy,G Nako,Joh Makini,Nikki wa Pili ambao ndiyo wanoonekana majukwaani na kusikika katika nyimbo zao.
Wakijibu maswali ya mwandishi wa blogu hii juu ya kuhusishwa kwa kundi la wesi na kupotea kwa kundi la hip hop toka Arusha lililofanya vema kwa masongi yake na style yao,Nack II Nako,baadhi ya wadau wamejibu:Kundi la Nako II Nako limekufa na kupotea tu kwasababu nyota wake tegemezi,G Nako na Lord Eazy wamechukuliwa.
Mwngine akasema: Nako II Nako limepotezwa na Weusi sababu nyota wake wamejikita zaidi katika shughuli za kundi la Weusi na wamesahau kundi lao la asili.
Mmoja akasema: sishangazwi na G Nako na Lord Eazy kulitupa Nako II Nako kwani ndiyo tabia ya wasanii wanapoelekea kwenye mafanikio,hugeukana na kufarakana.

0 comments:

Post a Comment