Kuna msemo usemao riziki popote,hayo yamejidhihirisha baada ya mrembo mmoja mwanafunzi wa chuo cha Boston Massachussets,Andele Lara,22,kuripotiwa kujiingizia pesa kwa kufanana kwake na star wa muziki duniani,Rihanna.
Lara ameongea na waandishi wa Daily Mail.
na kusema,nimeanza kugananishwa na Rihanna tangu anatoa wimbo ''Umbrella''.Rafiki yangu mmoja alikuja na jarida lililokuwa na picha ya Rihanna ukurasa wa mbele na kniambia umefanana sana na huyu,tangu hapo akaanza kujiremba,kujipodoa na hata kutengeneza mitindo ya nywele kama Rihanna na kuishi kama superstar.
Lala anasema kila anapopita mashabiki humshangilia na kumfata wapate saini wakizani ni Rihanna na hata akikataa si yeye wao huridhika na bado hung'ang'ania saini na kupiga naye picha.Amesema hata akiingia Club anapata ulinzi na hata watu wengi kumnunulia vinywaji wakijua ni Rihanna.Lara amesema kuna siku alikuwamo katoka club ambamo Chriss Bron alikuwamu,watu na mapaparazzy wakawa wanasubiri kwa hamu kuona kitachojiri.
Lara anasema amepata unafuu wa maisha kwa kufanana na Rihana,kwani tayari anatumiwa kuzitangaza bidhaa mbalimbali zikiwemo,vipodozi na hata viatu/raba ambapo analipwa zaidi ya dola 20,000 kwa mwezi.
Vipi Aristides ambaye amekuwa akifananishwa na Usher Raymond umefaidika na nini? Luda Criss,Snoop Lee na Snoop Dog,HK na Will Smith,Athumani Mush na Mwala,Elisa na Van Dame,Dj Dwhite na Fat Joe,Salum bonge na Sean Kingstone,Steve Nyerere,Babu Aayubu akiigiza viongozi.
Friday, November 21, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment