Mabondia Floyd Mayweather na hasimu wake Manny Pacquiao walihudhuria mechi ya mpira wa kikapu ya ligi ya NBA jana jumanne usiku,mechi iliyozikutanisha timu mbili za the Heat na the Bucks.Wakati mechi ikiendelea ghafla zikaonyeshwa picha za mabondia hao katika screen kubwa za ukumbini hapo wakifuatilia mechi hiyo na kuwafanya mashabiki kushangilia kwa sauti huku wakiwasihi mabondia hao wakutane ulingoni.
Moja kati ya watu wa karibu na mabondia hao amesema kwamba Pacquiao amesema Mayweather amempatia namba ya simu na amemshauri kama ni mpambano wao wauandae wenyewe.
Manny Pacquiao ameonekana ni mpenzi wa mechi za mpira wa kikapu hasa ligi ya NBA kwani alionekana pia wiki iliyopita katika mechi ya Clipperzs.
Floyd Mayweather Poses With His New Ferrari Enzo
Wednesday, January 28, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment