Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Thursday, January 29, 2015

Lil Wayne and Birdman
Lil Wayne anampeleka Birdman mahakamani.
Rappa huyo toka The Young Money,rasmi amefungua mashtaka mahakamani kumshitaki bosi wake na Cash Money akimtaka kumuachia huru kutoka katika lebo hiyo.
Mtandao wa TMZ umeandika, Wayne anadai Birdman amevuruga makubaliano yao kwa kuendelea kushikilia mamillioni ya madola yake sambamba nakuzuiwa kutoka kwa albamu yake mpya ya Tha Carter V.
Taarifa zaidi zinasema Cash Money hawapo tayari kumuachia Lil Wayne na wanavuruga makubaliano yaliyomo katika mkataba.
Lil Wayne ukiachilia mbali kutaka kuondoka Cash Money pia amesema anawadai kiasi kisichopungua dola millioni 51.
Katika madai yake mahakamani,Wayne amemtaka msimamizi wa kesi ampatie mkataba wa kumuhalalisha umiliki wa  Young Money recordings sambamba na wasanii f Drake, Nicki Minaj, Tyga, na wengine. 
Ikiwa Birdman atamlipa Wayne,Cash Money wataruhusiwa kuzindua albamu ya Tha Carter V. lakini watatakiwa kumlipa Wayne dolla millioni 8 kama malipo ya awali ya tangu alipoanza kuandaa albamu hiyo na kumlipa dolla millioni 2 akimaliza albamu.

0 comments:

Post a Comment