Mdau wa Hiphop,Marion "Suge" Knight ametajwa kuhusika katika tukio la watu wawili kugongwa na gari na mmoja kufariki papo hapo jana mchana (January 29) huko Compton, California. Mtandao wa kidaku wa story za mastaa huko America,TMZ,umeandika Suge Knight alihitilafiana na watu wawili alipokuwa katika utengenezaji wa filamu maeneo ya 1200 block West Rosecrans.Taarifa zinada wakati akiondoka kwa haraka eneo la tukio na kuingia katika gari lake na kuonoa gari kwa kasi na kwa bahati mbaya akawagonga watu watatu ambapo mmoja ni rafiki yake aliyekuja naye aliyekuwa akikimbilia kuingia upande wa abiria katika gari hilo aliyetambulika kwa jina la Terry Carter ambaye baadaye ilitangazwa amefariki .Wawili wengine walioumia ni sambamba na Cle "Bone" Sloane -- ambaye ameigiza katika filamu za "Training Day" na "End of Watch" ambao woe wapo hospitalini wakiendelea na matibabu. Mwanasheri wa Knight's bado hajathibitisha kama mteja wake ndiye aliyekuwa akiendesha gari hilo au lah.Kituo cha TV cha ABC cha nchini marekani kimesema inasemekana Suge Knight alivamiwa na watu wawili na ndipo alipoamua kukimbilia katika vyombo vya usalama.Dr. Dre na Ice Cube walikuwapo eneo la tukio lakini inasemekana waliondoka mapema baada tu ya shughuli za utngenezaji wa filamu kumalizika.
0 comments:
Post a Comment