Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Tuesday, January 20, 2015

Chanzo kimoja cha habari kimedai rappa "Jay Z" Carter akiwa na jopo la wawekezaji akiwamo mchezaji maarufu wa mpirwa wa kikapu wa timu ya NY Knicks, Carmelo Anthony wapo katika mazungumzo ya kutaka kukinunua kituo cha redio namba moja marekani cha cha  Hot 97 radio station,"Mtandao wa Mediatakeout.com umeripoti kwamba maongezi yapo katika hatua za awali lakini tayari pande zote mbili za wamiliki wa sasa na wanaotaka kununua wameshawaandaa wanasheria wao kwaajili ya kukamilisha mpango huo.
Ndani ya Kituo ch aredio cha Hot 97, wanapatikana madj na watangazaji maarufu kama,Ebro, Peter Rosenberg, Miss Info na Funkmaster Flex,ndicho kituo kinachotajwa kuutangaza zaidi muziki wa hiphop. 
Wiki iliyopita dj maarufu wa kituo hicho, Funkmaster Flex alimchana na alimjia juu rappa Jay Z kuhusu kumuibia mipango yake ya ubunifu wa tovuti ,swali linakuja ipi itakuwa nafasi ya dj huyo ikiwa rappa Jay Z akifanikiwa kukinunua kituo hicho na kuwa ndiyo bosi wake?


0 comments:

Post a Comment