Lil Wayne amekuwa katika harakati za kutaka kujitoa katika lebo inayommiliki ya Cash Money.
Bosi huyo wa The Young Money,Lil Wayne pia ametangaza kumshitaki bosi wa Cash Money,Birdman kwa kile anachokiita kumzuia kama mateka,kumcheleweshea kazi zake hasa albamu ya Tha Carter V na pia anamdai kiasi kisichopungua dolla millioni 8.
Sambamba na mashitaka hayo,Lil Wayne pia atafungua mashitaka zidi ya Birdman kuhusu uhalali wake wa kuwamiliki wasanii walipo katika lebo yake ya Young Money ambao ni Drake,Nicki, Christina Milian, Lil Twist na Mack Maine.
Weezy anaamini ikiwa ataondoka Cash Money ataondoka na wasanii hao kwasababu mkataba alisaini nao yeye kama bosi wa Young Money.
Kufuatia kucheleweshwa kwa albamu ya Tha Carter V,Lil Wayne ameachia mixtape inayokwenda kwa jina la Sorry 4 the Wait 2.
Tuesday, January 27, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment