Ndugu na wanafamilia wa mtoto pekee wa mastaa waimbaji,Whitney Houston na Bobby Brown,Bobbi Kristina Brown 21,wamekubaliana kuwaruhusu madaktari na wauguzi wa hospitali alipolazwa binti huyo,kumuondolea mashine maalumu za kumsaidia kupumua kwani tangu awekewe mashine hizo hajaonyesha dalili za kupata nafuu.
Bibi wa Bobbi,Cissy Houston ndiye aliyetoa wazo la kuruhusu mashine hizo kutolea siku ya tarehe 11 Feb tarehe sawa na siku aliyofariki mama yake,Whitney Houston mwaka 2012.
Wanafamilia wamesema kwa kufanya hivyo wanaamini ni kuwaunganisha mama na mwana kwa mara nyingine.
Bobbi Kristina, 21, amekuwa katika hali ya kutokujitambua tangu tarehe 31 Jan alipoookolewa akiwa amepoteza fahamu akiwa katika sinki la kuogelea nyumbani kwake.
0 comments:
Post a Comment