Week end iliyoisha rappa Meek Mill alikodisha jumba la kifahari la vioo lililokuwa limekodiwa na Justin Bieber hapo awali kwaajili ya pati maalumu ya kusherekea tuzo za Grammy.Pati ikiwa inaendelea walifika eneo la tukio baada ya majirani kuripoti kuna fujo na kelelle mtaani.
Mastaa kibao wakiwamo Nicki Minaj, French Montana, Khloe Kardashian, Chris Brown na Justin walihudhuria pati hiyo ambayo baadaye mida ya saa saba na nusu za usiku ilivunjika baada ya badhi ya waalikwa ambao ni washakaji wa rappa Meek Mill kuanzisha ugomvi uliopelekea kurushiana kwa makonde na hata kurushiana vitu.
Taarifa zinasema pati hiyo ilihudhuriwa na watu takribani 1000,na shughuli ya polisi kuwatawanya watu iligharimu zaidi ya masaa matatu.
Hakuna aliyekamatwa kutokana na vurugu hizo.
0 comments:
Post a Comment