Familia ya Carters wanapakia mabegi yao tayari kwaajili ya kuhamia Los Angeles.
Beyoncé na Jay Z wamehamua kuhama na kuhamisha makazi ya familia yao kutoka upande wa mashariki na kwenda upande wa magharibi wa Marekani (West Coast).Mtandao wa TMZ,umeandika,kwasasa familia hiyo inaishi katika hotel moja huko Beverly Hills wakiwa katika mchakato wa kutafuta nyumba watakayohamia kwani tayari wameshachagua maeneo ya kuishi huko westside L.A.,ambapo kuna maeneo kama Beverly Hills, Holmby Hills na Bel-Air.
Taarifa zaidi zinasema Jay Z na Beyonce tayari wameshaangilia baadhi ya nyumba lakini hawajaafikiana nazo.
Wakati wazazi wakitafuta sehemu ya kuhamia tayari wameshampatia mtoto wao Blue Iv shule ya program maalum ambayo atakuwa akilipiwa kiasi cha millioni 25 kwa mwaka.
0 comments:
Post a Comment