Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Monday, February 23, 2015

Kanye West
Yeezus alifanya mahojiano katika kipindi cha “The Breakfast Club” siku ya ijumaa.Bosi huyo wa The G.O.O.D. Music alipata muda wa kujadili mambo kadhaa yakiwemo bidhaa zake alizobuni za Yeezy Boosts mpaka aliyekuwa mpenzi wake, Amber Rose na pia ishu ya picha ya mkewe akiwa mtupu katika jarida na kama haitoshi mpango wake wa kufanya albamu ya pamoja na rappa Drake.
Kanye hivi karibuni ilibaki kidogo avuruge mambo wakati muimbaji Beck akitoa lisala ya kushukuru tuzo katika sherehe za utoaji wa tuzo za Grammy,Kanye alifikia kusema kumpa tuzo hiyo ya albamu bora Beck ni ukosefu wa nidhamu kwani ilistahili apatiwe Beyoncé.
Kanye anasema hakuwa sawa na hii ni baada ya kukiri kuisikiliza albamu ya Beck ambayo alisikiliza wakati akipata chakula cha usiku na muimbaji mahiri Taylor Swift.
Pamoja na kukiri albamu ya Beck ni nzuri,Kanye aliendelea kumtetea Beyoncé kwa kusema pamoja na hayo yote bado Beyoncé ni mkubwa na alistahili tuzo hiyo.
Kanye pia alipoulizwa kuhusu aliyekuwa mpenzi wake,Amber Rose kuhusu kile kinachoendelea katika mitandao alisema:Angekuwa katika mahusiano na Kim ndiyo aende kujihusisha na Amber anaamini asingekuwa na jina kama alivyo sasa.
Wakati Tyga has akikataa katika mahusiano ya kimapenzi na shemeji wa Kanye West,Kylie Jenner, Kanye ameongelea tofauti.Kanye amesema anadhani binti huyo mdogo wa umri wa miaka 17 toka katika familia ya Kardashian,amewahi sana mambo ya mahusiano lakini hashangai sana sababu kiumri hajapishana sana na Tyga,yapo mahusiano mengi yanaowahusisha watu waliopitana umri zaidi ya hao.
Kanye pia aliongelea mpango wake wa kufanya albamu ya pamoja na rappa Drake na tayari jina albamu lipo tayari,Wolves.

0 comments:

Post a Comment