Vanilla Ice alikamatwa kwa makosa ya wizi vifaa na fanicha na wanausalama jana (Feb 18) huko Lantana, Florida .
Rappa huyo ameiba thamani za ndani , bicycles na hita za swimming poll katika nyumba moja iliyotelekezwa iliyopo maeneo ya Sunshine State nyumba ambayo Vanilla Ice aliwahi kuikarabati na kuitumia katika vipindi vyake yva televisheni vya The Vanilla Ice Project mwaka 2010.
Mmiliki wa nyumba hiyo amesema hakutoa ruhusa kwa rappa huyo aliyewahi kutamba na kibao cha Ice Ice Baby kuchukua chochote katika nyumba hiyo hivyo kupelekea polisi kumchukulia hatua na kumfungulia mashataka ya wizi wa mali.
Baada ya polisi kufanya msako katika nyumba ya Vanilla Ice huko Palm Beach County walikuta baadhi ya vitu hivyo na kuvirudisha kwa mmiliki.
0 comments:
Post a Comment