Nicki Minaj yupo katika majonzi makubwa baada ya kuuwawa meneja wake wa ziara za muziki usiku wa kuamkia jana (Feb. 18) De’Von Pickett, 29.
Taarifa zaidi zinasema meneja huyo wa ziara za muziki za Nicki Minaj aliuwawa kwa kuchomwa na kisu katika ugomvi uliotokea katika bar huko Philadelphia inayofahamika kwa jina la Che Bar & Grill na kuendelea mtaani.
Mtu mwingine ambaye pia ni wa timu ya Minaj, Eric Parker, amejeruhiwa vibaya na anaendelea na matibabu hospitalini.
Watu hao wote wawili walikuwa katika mzoezi ya awali huko Philly kwaajili ya ziara ya muziki ya Nicki’ inayokuja ya “Pinkprint” European tour, ambayo imepangwa kuanza mwezi March tarehe 16 huko Sweden.
Nicki alitangaza habari hizi za kuhuzunisha katika akaunti yake ya Twitter kwa kuandika: “Two members of my team were stabbed last night in Philly. One was killed. They had only been there for two days rehearsing for the tour,” she said.
Kufuatia taarifa hizo mastaa kibao wakiwamo Rihanna, Pusha T, Fabolous, K. Michelle, Tiara Thomas walituma salamu za pole kwa wahusika.
Tazama picha ya De Von Pikett wa kushoto hapo chini:
0 comments:
Post a Comment