Mdau wa hiphop Suge Knight kuhukumia kifungo cha maisha kufuatia tukio la siku ya alhamisi la kumgonga rafiki yake,Terry Carter na kupoteza maisha huko Compton Marekani wakati wa utengenezaji wa filamu.
Knight pia anashtakiwa kwa makosa mawili likiwemo la kugonga mtu na kukimbia na kufanya vurugu akiwa chini ya uangalizi kisheria kwa kesi nyingine inayomkabili.
Taarifa zaidi zinasema dhamana ya dolla millioni 2 iliyokuwa awekewe Suge imekataliwa kwasababu ambazo zimeelezewa ni pamoja na hatari ya kupoteza ushahidi wa tukio zima.
Suge kupandishawa kizimbani siku ya jumanne.
Shahidi mmoja aliyekuwapo katika eneo la tukio alisema,Suge aliingia katika gari lake na kuanza kurudi nyuma kwa kasi akitaka kuwagonga watu aliohitilafiana nao na ndipo kwa bahati mbaya
akawagonga watu watatu na kupoteza maisha ya mmoja kati yao ambaye ni rafiki yake. Wakili wa Suge amesema mteja wake alifanya ajali kwa bahati mbaya baada ya kuondoa gari kwa kasi akikimbia kuvamiwa.
Mtandao wa TMZ umesema kesi ya Suge itategemea pia na ushahidi wa video.
0 comments:
Post a Comment