YMCMB star,Tyga alitinga katika kituo cha redio cha Power 105.1 katika kipindi cha The Breakfast Club jana (February 16) kujadili mambo kadhaa yakiwemo mahusiano yake na binti mdogo toka familia ya The Kardashian,Kylie Jnner na utata wake na rappa mwenzake toka YMCMB,Drake.Akiongea na mtangazai wa kipindi cha The Breakfast Club kabla ya kuanza kujibu maswali,Tyga alianza kujielezea kwa kusema:Yeye si mtu kuanika mambo yake binafsi hadharani.sipo katika mahusiano na Kylie [Jenner],ningependa jamii itambue hilo,na wala sijatengana na familia yangu kwaajili ya Kylie,Tyga ameongeza kusema mahusiano yake yeye na mama wa mtoto wake,Chyna, yaliisha inakaribia mwaka sasa.Tyga amesema waliposhindwana walikubaliana watengane ila watashirikiana katika malezi ya mtoto wao.Tyga pia amesema hashangazwi na uvumi huo kwani katika utamaduni wa watu weusi ukiwa karibu na mtu wa jinsia tofauti basi unahesabiwa unajihusisha naye kimapenzi ila ni tofauti na tamaduni za wenzetu weupe,ikiwa ni rafiki mtakuwa marafiki tu wakweli na mengineyo.
Rappa Tyga pia amezungumzia ugomvi wake na rappa mwenzake toka Young Money,Drake na kusema ishu yake ni tofauti na ishu ya Cash Money, Tyga pia hakutaka kuzungumzia hali ya sintofahamu inayoendelea kati ya Cash Money na Lil Wayne.Tyga amesema amefanya mengi na Cash Money ikiwemo kuuza zaidi ya singo millioni 11 bila kupewa nguvu ya msukumo katika radio,amesema ameongea na mmiliki ambaye ni Birdman na ilikuwa wamalizane mwezi uliopita lakini anaona kimya hivyo haelewi kwanini Cash Money wanang'ang'ania.
Na alipoulizwa kuhusu Drake alisema,siwezi kulumbana naye wala sina beef naye ila namchana kufuatia kukosa uhalisi kutokana na tabia yake ya kupenda kujianika yeye na mambo yake na hata muziki wake.
0 comments:
Post a Comment