Rappa na bosi wa Bad Bys,Diddy yupo mikononi mwa polisi kwa kumshambulia kocha wa timu ya football.
Mtandao wa kidaku wa habari za mastaa America, TMZ,
umeandika,polisi walifika uwanjani na kumtia Diddy mikononi na kwenda naye kituo cha polisi baada ya mwamba huyo wa Hiphop kumtetea mwanaye ambaye ni mchezaji wa American football wa UCLA siku ya jumatatu June 22.
Taarifa zaidi zimedai kuwa chanzo cha mtafaruku huo ni pale kocha msaidizi wa wa timu anayochezea mtoto wa Diddy,Justin Combs,alipoonekana akimkemea mtoto huyo ndpo Diddy alipolazimika kuingia uwanjani na kumvaa kocha huyo.
Mpaka sasa Diddy bado yupo selo.
Tuesday, June 23, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment