Rapa The Game amesema bado anakula mkwanja kutokana na kazi zake alizofanya solo na hata alizozifanya na kundi lake la zamani,G-Unit.
The Gam ametamka alipohojiwa na waandishi alipohudhuria sherehe za BET Awards afterparty, The Game bado ananufaika na jasho lake alilolitoa wakati yupo na kundi lake la zamani kwani anapata mgawo wa mauzo wa kazi zao ambazo bado zinaendelea kununuliwa.
Rappa The amesema amejipatia kiasi kisichopungua dolla millioni 30 toka aachane na kundi la G-Unit .
The Game hakujumuishwa wakati kundi lake la zamani lilipowakutanisha wanachama wake mwaka 2014 na kutumbuiza katika tamasha la Summer Jam kutokana na rappa huyo kutokuwa na maelewano mazuri na bosi wa G-Unit,50 Cent.
Rappa huyo toka pande za Los Angeles yupo studioni akimalizia albamu yake ya The Documentary 2..
Friday, July 3, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment