Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Monday, August 17, 2015

Straight Outta Compton

Filamu inayoelezea maisha ya waliokuwa wakiunda kundi la N.W.A,Straight Outta Compton imezinduliwa siku ya ijumaa na imevuka makadirio kimauzo na kushika namba moja.
Filamu hiyo iliyoongozwa na director maarufu F. Gary Gray ambaye pia alitengeneza filamu zilizoganya vizuri kama Friday (1995),Set It Off  waigizaji aliekuwa mfanyakazi wa benk, Frankie aliyeigiza Vivica A. Fox na rafiki yake Kimberly Elise,single mother;Queen Latifah aliyeigiza kama Cleo, Jada Pinkett aliyeigiza kama Stony (1996) ,The Negotiator (1998),Murder was the Case (1995),alishiriki pia kutenegeza Italian Job 2003,Be Cool (John Travolta) 2005.
Director amejitengezea rekodi mpya baada ya Filamu yake hiyo mpya kuvuka malengo ya uuzwaji na kuipiku hata filamu ya American Pie 2 ya mwaka 2001 iliyouza dola millioni 45.1 .
Mbali na kuvunja rekodi ya mauzo pia imekuwa filamu iliyotengeneza historia katika funguzi zake ukilinganisha na filamu zingine zinazohusu muziki.kama filamu ya minem’s 8 Mile ($51.2 million)  2002.
Filamu hiyo ya Compton imekaribia kufikia faida mara mbili ya ghrama za uengezaji wake kwani uligharimu dolla millioni 29. Ice Cube na Dr. Dre wmeshiriki kikamilifu katika utengenezaji wa filamu hiyo sambamba na mjane wa rappa Eazy-E,Tomica Woods-Wright.
Mastaa kibao wa muziki wameunga mkona kuitazama filamu hiyo ambapo  Nicki Minaj na boyfriend wak, Meek Mill walikodisha jumba la sinema ili watizame wao na timu yao.

Filamu ya Straight Outta Copmpton inayohusu maisha halisi ya waliokuwa wanachama wa kundi la muziki wa hiphop la N.W.A, ilizinduliwa rasmi katika majumba ya sinema siku ya ijumaa tarehe 14 na tayari imeuza kiasi cha dolla milioni 56.1.

0 comments:

Post a Comment