Drake amekuwa na mwaka mzuri,baada ya mafanikio kadhaa kupitia kazi zake za muziki na matangazo hivi karibuni ameachia collaborative mixtape na rappa Future iliyompelekea kufikisha nyimbo 100 katika chati za Billboard Hot 100 ikiwa ni miaka 6 tu imepitya tangu atambulike katika ulimwengu wa muziki.( amekadiriwa kuwa nyimbo bora 16 kila mwaka )
Rappa huyo toka Toronto alikuwa na nyimbo 92 kabla ya kutoa hii mixtape siku ya jumapili iliyopelekea kuingiza nyimbo 8 kwa charts hizo za Billboard.
Drake amefikisha nyimbo 100 katika chati za Billboard rekodi ilikuwa inashikiliwa na waimbaji / vikunde vinne tu tangu mwaka 1958.
Kundi la The Glee cast ndiyo linaloongoza kuwa na singo nyingi zaidi katika chati za Billboard Hot 100 (kwa kuwa na zaidi ya nyimbo207), anayefuata ni Lil Wayne (127), Elvis Presley (108),na sasa Drake (100).
Mixtape hiyo inayokwenda kwa jina la "What a Time to Be Alive" imeshika namba 1 katika chati hizo bora kabisa duniani za Billboard 200.
0 comments:
Post a Comment