Jay Z ni rappa mkubwa na tajiri anayetajwa kuwa na utajiri unaozidi dolla millioni 500.
Wakati hapa Bongo watu kukaa VIP ama backstage wanaona ni ujuko,Siku ya jumamosi usiku Jay Z aliwashangaza walimwengu pale alipoamua kujichanganya na maelefu ya mashabiki wa kawaida waliokuwa wamefurika kumuangalia Beyoncé akitumbuiza katika tamasha linalofanyika kila mwaka la Made in America.
Jazy Z pamoja na kujichanganya na kuwa karibu na watu wengi inasemekana hawakumtambua haraka kwani wengi walikuwa wameelekeza macho jukwaani kumtazama Beyonce anavyoshambulia jukwaa.
0 comments:
Post a Comment