Akon ambaye amewasaini mastaa kama T-Pain na Lady Gaga na wakali wengine kibao katika lebo zake za Konvict Muzik na KonLive ameelezea sababu juu ya kwanini hakumsaini rappa mahiri Drake ambaye alipelekeawa na muimbaji mcanada mwenzake, Kardinal Offishall .
Akihojiwa katika mahojiano na Montreality Akon alisema,moja kati ya sababu za kutomsaini Drake wakati huo kwanza alikuwa hana uwezo kama alionao sasa,alikuwa mtu wa aibu na hata aliposikiliza moja kati ya ngoma zake ikiwemo ‘Best I Ever Had,haikuwa na ubora huo ila ashangai kwani wakali wengi katika sanaa ya music wanaendelea kuiva na kuonekana wazuri zaidi wanavyokua wakubwa.
Akon amemaliza kwa kusema ,anadhani kujiamini kumekuwa na ametanuka kiujuzi ndiyomaana mnayaona haya ayafanyayo.
Thursday, October 1, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment