Kumekuwa na habari iliyosambaa kwamba muimbaji mahiri toka lebo ya Mavins,Tiwa Savage kuwa yu mbiono kusaimniwa na lebo kubwa duniani inayomilikiwa na rapa Jay-Z,Roc Nation.
Bosi wa Mavins Records ya Nigeria,Don Jazzy na muimbaji wake Tiwa Savage wamekutana na Jay Z katka makao makuu ya Roc Nation huko mjini New York.
Taarifa zaidi zinasema kwamba dili hilo limeonyesha muelekeo wa kukamilika tangu ndugu wa Jay-Z’ bw Brian “Bee-High” Biggs atembelee makao makuu ya studio za Mavin huko Lagos Nigeria mwaka jana.
Tiwa Savage ambaye kwasasa yupo katika mchakato wa kuitangaza albamu yake ya "R.E.D" pia ametajwa kutumbuiza katilka tamasha la Made in America mwezi September,ambapo Rihanna iametajwa kuongoza onyesho hilo kwa mwaka huu.
Tiwa Savage ikiwa atasainiwa Roc Nation yenye ofisi kubwa mijiniNew
York, London na Los Angeles,atakuwa ameungana katika familia ya mastaa kama
Rihanna, Big Sean, DJ Khaled, Kanye West na wakali wengine kibao.
0 comments:
Post a Comment