Waswahili husema hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho,japo huwa haijulikani mwisho gani.
Hayo yamejidhihirisha baada ya staa wa kike wa muziki wa kufoka Iggy Azalea kutajwa kumwagana na mpenzi wake ambaye ni staa wa mpira wa kikapu wa ligi ya NBA, Nick Young ikiwa ni mwaka moja tangu waingie katika mahusiano.
Rapa mwenye asili ya Australian,Iggy Azalea ndiye aliyeweka wazi juu ya kuvunjika kwa mahusiani yao kupitia ukurasa wake wa Instagram akijielezea kwamba hawezi kuendelea kimapenzi na Nick Young sababu hamuanini tena.
Iggy aliandika:
"Unfortunately
although I love Nick and have tried and tried to rebuild trust in him -
It's become apparent in the last few weeks that I'm unable to. I
genuinely wish Nick the best. It’s never easy to part ways with the
person you planned your entire future with, but futures can be rewritten
and as of today mine is a blank page.” .
0 comments:
Post a Comment