Muimbaji wa muziki wa rnb nchini tanzania ambaye kwa sasa anafanya vizuri na record yake mpa Wivu,amesema anatoa nafasi kwa wasanii wenye uwezo wa kuandika muziki wa namna yake wamuandikie kisha atawalipa kama zitakuwa katika ubora unaohitajika.Akiongea katika mahojiano na watangazaji wa kipindi cha Red Carpet cha Radio One Stereo,Jux amesema mara zote amekuwa akiwalipa vizuri wanaomuandikia nyimbo na kama haitoshi hutoa heshima kwao na kuwataja kama wamemuandikia.Sababu kubwa ya kutoa nafasi kwa wasanii kumwandikia ni kutaka kupata Ladha tofauti na kutoa fursa kwa wasanii kama sehemu m badala ya kuwaingizia kipato.
Monday, August 22, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment