Uchaguzi wa kihistoria umefanyika huku kukiwa na ushindandi mkali baina ya wagombea Bi Hillary Clinton dhidi ya Bw Donald Trump aliyeibuka mshindi.
Mgombea kupitia chama cha Democratic Hillary Clinton
alitangazwa kushindwa na Donald Trump kufuatia mgombea huyo wa Republican kufikisha kura za wajumbe 270 zilizokuwa zikihitajika.
Bw Trump ameshinda majimbo mengi muhimu kama Ohio, Florida, na North Carolina, ingawa Bi Clinton alishinda Virginia.
Taarifa zaidi ni kwamba gombea wa Republican Bw Trump ameshinda majimbo mengi ya kusini mwa
Marekani naye Bi Clinton akashinda majimbo ya kaskazini mashariki mwa
nchi hiyo, kwa mujibu wa makadirio ya shirika la utangazaji la ABC News.
Bi Clinton amempigia simu Bw Trump kumpongeza kwa ushindi wake.
Uchaguzi umemalizika huku wengi wakibakiwa na sintofahamu na kuhoji hali itakuwaje kwa mastaa waliojiapiza kama Jay Z aliyesema “He cannot be my president, he cannot be our president!” katika concert ya kuwashawishi watu wamchague bi Hillary Clinton huko Cleveland.
Mwingine ni muigizaji mahiri wa filamu marekani bw Samuel Jackso aliyesema :
“If that **** becomes president I will move my black ** to South Africa.”
Wednesday, November 9, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment