Kanye West alipelekwa hospitali kwa gari maalumu la kubebea wagonjwa na kulazwa katika hospitali ya Ronald Reagan UCLA Medical Center Los Angeles jumatatu (Nov. 21) baada ya daktari wake kumpima na kugundua anahitaji kupumzishwa kufuatia uchovu wa kutopumzika na kulala kunakosababishwa na ziara yake ya ST Pablo tour.
Polisi wa LAPD wamesema hali ya Kanye West haihusiani na tukio lolote ama shambulizi ni mswala ya afya yake tu na hii ni baada ya mashabiki kuhoji labda kitendo cha kurusha madango kwa vigogo kama Jay Z,Obama,Donald Trump nk.
Kabla ya tukio la kupelekwa hospitali na kulazwa imeripotiwa Kanye alikatisha maonyesho mawili kwa matatizo ya kukaukiwa sauti.Taarifa zaidi zinasema kambi ya Kanye imehairisha ziara zilizobaki na kwa kuhairisha huko basi rapa huyo atakosa kisai kinachichotajwa kuwa ni dola millioni 10.
0 comments:
Post a Comment