Siku ya jumanne December 13, 2016, Kanye West alikutana na billionaire ambaye ni raisi mteule wa US , Donald Trump katika jengo lake la Trump Tower.
Kanye West kukutana na raisi mteule wa US , Donald Trump kumezua mzozo kwa watu wengi hususan wasanii wenzake mmoja wapo ni mshikaji wake wa karibu John Legend.
Akiwa katika interview waandishi wa jarida la Clique John Legend amesema Kanye amesema haamini kama kweli alikwenda kukutana na raisi huyo kujadili mustakabali wa nchi na wanachi wa hali ya chini na muhimu kama waalimu bali ilikuwa kutafuka kiki (publicity stunt).
John Legend pia amesema alikasirishwa na kauli ya Kanye West kusema kama angepiga kura angempigia Trump.
0 comments:
Post a Comment