Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini anayetamba na wimbo wake mpya Mazowea aliomshirikisha Mwana Fa,Bill Nas ameweka wazi alichokimaanisha katika wimbo wake huo mpya.
Akiongea na Dj Show ya Radio One msanii BiLL Nas amesema Mazowea inahusu wale wanaomtazama kikawaida na kumchukulia poa kamba hatokuwa Billnas yuleyule bali atakuwa anabadilikabadilika hivyo waliojua atazoeleka basi wamechelewa.
Bill Nas pia amekanusha taarifa zinazosambaa zinazosema ametoa wimbo Mazowea kuwapiga kijembe waliomuibia vifaa vya gari yake ambayo taarifa inasema wazee wa kupukutisha wameipitia na kuimasage na kusema wimbo huo aliuandaa zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Monday, January 30, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment